ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 26, 2010

Gaddafi aitisha jihad dhidi ya Uswizi



Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amewataka Waislamu kuanza vita vya Jihad dhidi ya Uswizi.
Kanali Gaddafi anadai kwamba nchi hiyo imeanzisha kampeini ya kuharibu misikiti baada ya kura ya maoni nchini humo mwezi Novemba, kuidhinisha kupigwa marufuku kwa ujenzi wa minara katika misikiti ya Uswizi
Kanali Gaddafi pia ametaka waislam kote duniani kususia bidhaa za Uswizi. Kiongozi huyo wa Libya ameyasema hayo mjini Benghazi wakati wa kuadhinisha siku ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamed.
Kumekuwa na mzozo wa kidiplomaia kati ya Libya na Uswizi tangu mwana wa Kanali Gaddafi pamoja na mkewe kukamatwa nchini humo kwa tuhuma za kumdhulumu mjakazi.
Wiki iliyopita, Libya iliwapiga marufuku raia wa muungano wa Ulaya kupata vibali vya kuzuru nchi hiyo. Hiyo ilifuatia hatua ya Uswizi kutoa orodha iliyowawekea vikwazo raia 188 wa Libya, ikiwa ni pamoja na Kanali huyo na watu wa jamii yake.

No comments: