ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 28, 2010

Capello: Terry hatakuwa nahodha chini yake


Kocha wa England Fabio Capello amesema John Terry kamwe hatorejea kuwa nahodha wa timu hiyo chini ya uongozi wake.
Terry alivuliwa unahodha baada ya tuhuma zinazohusu maisha yake binafsi huku Rio Ferdinand akichukua nafasi yake.
Capello amesema hadi katika Kombe la Dunia, Terry hatakuwa nahodha tena. Baada ya Kombe la dunia, iwapo atendelea kuwa kocha wa England pia hadhani kama Terry ataweza kuwaongoza wenzake.
Ameongeza kusema Capello, "ninataka nahodha kuwa mfano mzuri kwa vijana wadogo. Kile alichofanya sio kizuri, nimemueleza hilo na ameelewa."
Terry, mwenye umri wa miaka 29, bado ana imani atarejea katika nafasi yake ya unahodha, lakini Capello anahisi hafai tena kuwa nahodha kutokana na kumuendea kinyume mchezaji mwenzake wa England Wayne Bridge.

No comments: