Meneja wa United Sir Alex Ferguson amesema mlinzi huyo wa kati alikuwa akijisikia maumivu ya kichomi mgongoni alipokuwa mazoezini na haingekuwa jambo la busara kumchezesha siku ya Jumanne na West Ham.
Ferguson ameongeza kubainisha kwamba Ferdinand alikuwa na matatizo hayo siku za nyuma na akasema hatacheza siku ya Jumapili.
Ferdinand, mwenye umri wa miaka 31, mapema mwezi huu alichukua nafasi ya unahodha wa England kutoka kwa John Terry lakini huenda asiwemo katika kikosi kitakachotangazwa siku ya Jumapili kwa ajili ya pambano na Misri.
No comments:
Post a Comment