ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 27, 2010

Nigeria yampata Msweden Lagerback


 Nigeria imemteua kocha wa zamani wa Sweden Lars Lagerback kuwaongoza katika Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwezi wa Juni.
Lagerback aliteuliwa akiwa amewapiku Glenn Hoddle na Sven-Goran Eriksson, ambao wote walikuwa waiinyemelea kazi hiyo.
Msemaji wa Shirikisho la Soka la Nigeria Ademola Olajire amesema Hoddle na kocha wa zamani wa Senegal Bruno Metsu waliwavutia wakati wa mahojiano.
Lakini akaongeza Lagerback kwa sasa amekwishatia saini mkataba wa miezai mitano kuifundisha Nigeria kuelekea katika Kombe la dunia.

No comments: