ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 27, 2010

Tetemeko kubwa latokea Chile

mmoja wa watu waliojeruhiwa katika tetemekoWatu kumi na sita wanaarifiwa kufariki dunia kufuatia temeko kubwa la ardhi lililo na kiwango cha takriban alama tisa katika vipimo vya matetemeko ya ardhi nchini Chile.
Tetemeko hilo linasemekana kuwa la nguvu zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Watu katika mji mkuu Santiago, zaidi ya kilomita mia tatu kutoka katika kitovu cha tetemeko hilo wameelezea kuamshwa na mtikisiko huo ulioangusha vyombo na meza.
Nyaya za simu na umeme pia ziliharibika.
Rais wa Chile, Michelle Bachelet, amesema kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka huku watu wakishauriwa kubaki nyumbani.
Idara ya Marekani inayotoa tahadhari kuhusu matetemeko, imesema kiwango cha bahari kilionyesha ishara za tsunami, lakini haikuweza kupata ufafanuzi juu ya ukubwa wake.
Tetemeko hilo pia lilisikika katika maeneo ya Andes nchini Argentina.

No comments: