ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 27, 2010

Rooney huenda akapumzika Kombe la Carling


Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson anafikiria kumpumzisha mshambuliaji wake hatari Wayne Rooney katika mchezo wa fainali ya Kombe la Carling na Aston Villa.
Rooney tayari amekwishapachika mabao 11 katika michezo minane iliyopita, lakini Ferguson anapima iwapo mshambuliaji huyo anahitaji kupumzika au la.
Ferguson amesema bado anafikiria. Tatizo Rooney anahitaji kucheza kila mechi.
United wiki mbili zijazo watakabiliana na AC Milan katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na pia wanajinoa kwa ajili ya kutetea taji la Ligi Kuu ya England wakichuana na Chelsea.
Ferguson anakabiliwa na kibarua kigumu kuchagua timu kwa ajili ya mechi na Aston Villa, ambao wanakiu ya kumaliza ukame wa miaka 14 bila ya kombe.

No comments: