ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 15, 2010

TBL yapandisha bei ya bia

KAMPUNI ya Bia nchini (TBL) imetangaza kupandisha bei ya bia rejareja na jumla kuanzia kesho Jumanne.

TBL imeagiza kwamba, nyongeza ya bei ya chupa moja kwa mnywaji isizidi sh 100.

Kampuni hiyo imesema, bei imeongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei ya malighafi, kupanda gharama za uzalishaji, usafiri, mafuta, na mabadiliko ya kiwango cha kubadilisha fedha.

Baadhi ya bia zenye ujazo wa mililita 500 zilizokuwa zikiuzwa mtaani sh 1,300 sasa zitakuwa sh 1,400 ambazo ni Safari lager, Kilimanjaro, Bingwa, Ndovu special Malt na balimi.

Kwa baadhi ya bia zenye ujazo wa mililita 330 ambazo zitauzwa sh 1,200 kwa rejareja ni Safari Lager, Kilimanjaro, na Tusker Lager

1 comment:

Anonymous said...

Isiwe tabu,tutaponea uwanja wa fisi