Advertisements

Monday, February 15, 2010

Trapattoni awatolea nje Nigeria


Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Italia (Ansa) meneja wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland Giovanni Trapattoni amekataa kuifundisha timu ya taifa ya Nigeria.
Trapattoni amekiri ametakiwa kwa kazi mbalimbali, lakini anayo miaka miwili zaidi na timu ya Ireland na hana matatizo na kazi yake ya sasa.
Taarifa hizi zimekuja baada ya mshauri wake, Domenico Ricci, kukaririwa akisema Trapattoni huenda angependa kuifundisha Nigeria.
Ricci ameongeza kusema kwamba Trappatoni pia amekataa kazi ya kuifundisha Ivory Coast.

No comments: