Beckham amimina sifa kwa Wayne Rooney ![]() | ||||
David Beckham amemsifu Wayne Rooney kuwa ni mmoja wa wachezaji bora duniani baada ya kuiwezesha Manchester United kuingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Mshambuliaji huyo wa England alipachika mabao mawili, kama alivyofanya katika mchezo wa kwanza na kuwalaza AC Milan 4-0. Beckham amesema: "Wayne ana kipaji cha pekee. Ameendelea kumsifu akisema"Hakuna ubishi ni moja ya wachezaji hodari duniani kwa wakati huu ukimchanganya na Cristiano Ronaldo pamoja na Lionel Messi." | ||||

No comments:
Post a Comment