ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 11, 2010

Biden ajaribu kuzuia uhasama kuzidi

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden

Makao ya Wayahudi
Zaidi ya Wayahudi laki tano wanaishi katika makao zaidi ya 100 Palestina

Joe Biden, makamu wa rais wa Marekani, amesema haifai kabisa kuchelewesha mashauri ya amani ya Mashariki ya Kati, licha ya mzozo uliopo kuhusiana na walowezi wa Israel kujenga makao zaidi Jerusalem ya Mashariki.
Bw Biden alirudia tena matamshi yake ya kupinga uamuzi wa uamuzi wa ujenzi huo, lakini alielezea kufurahishwa na jibu la waziri mkuu Benjamin Netanyahu kuhusu mzozo huo.
Vile vile alielezea kwamba Marekani "haina rafiki bora zaidi ya Israel".
Halmashauri ya Palestina awali ilikuwa imeelezea kwamba mashauri ya amani yatakuwa "magumu mno" iwapo mipango ya ujenzi wa makao hayo ya Wayahudi haitafutiliwa mbali.

No comments: