![]() | ||||
Rais wa Sudan Omar Al Bashir ametishia kuwafukuza wachunguzi wa kigeni wa uchaguzi mkuu na akafutilia mbali pendekezo walilotoa la kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi ujao. Rais Bashir amesema kuwa iwapo wachunguzi hao wataendelea kuingilia mambo ya ndani ya nchi yake atakata vidole vyao, awakanyage kanyage na kisha kuwatupa nje ya nchi yake. Wiki iliyopita maafisa wa shirika la uchunguzi la Marekani American Carter Center walipendekeza kucheleweshwa uchaguzi huo japo kwa muda ili kukamilisha maandalizi. | ||||

No comments:
Post a Comment