ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 14, 2010

"LUNYASI" yanyakua ubingwa Tanzania


 [kocha.JPG]
kocha wa Simba Patrick Phiri akibebwa juu.juu kwa furaha ya kuchukua ubingwa kabla ligi kuisha,picha kwa hisani ya Michuzi
Klabu ya soka ya Simba ya Dar es Salaam, Tanzania imenyakua ubingwa wa ligi kuu, huku zikiwa zimesalia mechi mbili kabla ya kumaliza msimu.
Simba imefikisha pointi 56 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Yanga nayo ya Dar es Salaam imechukua nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 ikiwa nayo imebakiza mechi tatu.
Simba imetwaa ubingwa kwa kushinda mechi 18 na kutoka sare mechi mbili.
Hii ni mara ya kwanza nchini Tanzania, kwa timu kuchukua ubingwa bila kufungwa hata mechi moja.
Simba imebakiza mchezo dhidi ya Yanga na Mtibwa Sugar.

No comments: