
Aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Winnie Mandela, amekanusha kumtuhumu rais huyo wa zamani katika mahojiano na gazeti moja la Uingereza. Bi Mandela amesema mahojiano hayo yanayomtuhumu bw Mandela kuwatelekeza watu weusi yaliyochapishwa na gazeti la Evening Standard ni ya uzushi. Makala iliyobeba mahojiano hayo iliandikwa na Nadira Naipul, ambaye ni mke wa mshindi wa tuzo ya Nobel, VS Naipul. Bw na Bi Mandela ambao wote walikuwa viongozi katika harakati za ukombozi wa Afrika Kusini, walitalikiana mwaka 1996. Makala hiyo ilimkariri Bi Mandela akisema mume wake 'aliingia mkataba usiowasaidia watu weusi'. |
No comments:
Post a Comment