Madenti wapigishwa donee kukodisha Walimu!
Wakati Skonga ya Sekondari Iligala iliyopo mwambao wa Kusini wa ziwa Tanganyika ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu uongozi wa shule hiyo umekuwa ukiwachangisha fedha madenti kwa ajili ya kupata walimu wa kukodi.
Imeelezwa kuwa kwa sasa shule hiyo ina mateacher wawili tu wanaofundisha kati ya walimu saba walioajiriwa hali inayowawia vigumu walimu hao kufanya kazi wenyewe.
Kati ya walimu hao saba walimu watatu wako masomoni jijini Mwanza na walimu wawili wagonjwa.
Kutokana na hilo alisema kuwa uongozi wa shule chini ya Bodi ya Shule hiyo umeamua kuwatafuta wahitimu wa kidato cha sita (voda fasta) kusaidia kazi hiyo na kuingia nao mkataba.
Hata hivyo pamoja na nia hiyo njema lakini skonga hilo lnakosa fungu kwa ajili ya kugharamia posho za mateacher hao wa kukodi na hivyo kulazimika kuwachangisha madenti kwa ajili ya kupata posho za walimu hao wa kukodisha.
Kwa upande wao wanafunzi wa shule hiyo walisema kuwa uchangishaji wa fedha kwa ajili ya posho za walimu wa kukodisha ni mzigo mkubwa kwa wazazi wao na pia inachangia kushusha taaluma.
Diwani wa Kata ya Ilagala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata Hamisi Mkwavi alisema kuwa hali hiyo kwa sasa haiepukiki kutokana na tatizo kubwa la uhaba wa walimu na ndipo wameweza kuchukua njia hiyo kusaidia hali hiyo.
No comments:
Post a Comment