ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 29, 2010

Milipuko yautikisa mji wa Moskow
 
abiria walionusurika
manusura wa mlipuko
Wakuu wa Urussi wanasema kuwa zaidi ya watu 30 wameuawa katika milipuko miwili iliyotokea ndani ya vituo vya treni za chini(metro).
Meya wa mji wa Moscow amesema baada ya milipuko hiyo kuwa wanawake waliojitolea mhanga maisha yao ndiyo waliofanya kazi hiyo. Wakati huo huo taasisi za usalama zimesema kuna uwezekano milipuko hiyo ikawa na uhusiano na makundi ya wakereketwa wa kaskazini.
Tathmini ya mhariri wa BBC wa masuala ya usalama ikitegemea habari za hapa na pale ni kwamba mtazamo rasmi wa Urussi ni kwamba wakereketwa wa majimbo ya kaskazini wameamka.
Na endapo habari hizi zitasahihishwa na jinsi milipuko hii ilivyofanyika kwa mpango wa kiwango cha juu basi haya ni mashambulizi makali kuwahi kutokea tangu mwezi february mwaka 2004. Wakati huo pia mlipuko ulitokea wakati watu wa kutoka kazini na mlipuko kutokea ndani ya kituo cha treni. Wakati huo kama leo, mwanamke alihusishwa.
Tukio la leo ni fedheha kwa wakuu wa Urusi ambao kwa mda sasa wamekuwa wakijigamba kufanikisha vita dhidi ya ugaidi.

No comments: