Rais Obama atia saini sheria ya kihistoria | |||||
Rais Barack Obama ameidhinisha sheria muhimu ambayo itatoa bima ya afya kwa Wamarekani wapatao milioni 32. Kwenye sherehe iliyoandaliwa katika ikulu ya White House, Rais Obama alitoa mfano wa mamake mzazi ambaye “aliendelea kubishana na makumpuni ya kutoa bima huku akiwa anaugua saratani”. “Baada ya jitihada za karibu karne nzima, baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mjadala, baada ya kura zote kuhesabiwa, leo hii mabadiliko kuhusu bima ya afya yanaidhinishwa kuwa sheria Marekani,” alisema Rais Obama. Viongozi wa chama cha upinzani cha Republican wamepinga vikali mswada huo wakisema utagharimu pesa nyingi. Pindi tu baada ya mswada huo kutiwa saini, wakuu wa sheria 12 wa chama cha Republican na mmoja wa Democrat walianza mchakato wa kuishtaki serikali kuu wakisema mswada huo unakiuka katiba ya Marekani | |||||
ANGALIA LIVE NEWS
Tuesday, March 23, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment