Wayne Rooney amewataka mashabiki wa soka wa England wasimzomee John Terry katika mchezo wa kirafiki na Misri siku ya Jumatano.Mshambuliaji huyo wa Manchester United amewataka mashabiki kumuunga mkono Terry aliyevuliwa unahodha wa England mwezi uliopita kutokana na tuhuma za kuwa na mpenzi nje ya ndoa.
Rooney amesema"Terry sio nahodha tena wa England, lakini bado ni mchezaji muhimu na kiongozi mzuri."
Rooney pia amesema yupo tayari kwa mchezo wa Jumatano utakaochezwa uwanja wa Wembley licha ya kusumbuliwa na maumivu ya goti.
Mechi ya Jumatano itakuwa ni ya kwanza kwa England tangu zilipoibuka kashfa za Terry za kuwa na uhusiano na mpenzi wa zamani wa Wayne Bridge aliyewahi kuichezea pia Chelsea na England ambaye kwa sasa yupo na timu ya Manchester City.
No comments:
Post a Comment