ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 28, 2010


Utalii wahamia Arushaa!!


Mkoa wa Arusha umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa fainali za Kanda ya Kaskazini za Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu zitakazorindima Aprili 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa hoteli ya kitalii ya Kibo Palace jijini humo.

Akizungumzia maandalizi ya shindano hilo, Mkurugenzi wa Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini, Pendo Simwita, alisema kuwa kila kitu kinakwenda vema na kuziomba kampuni na watu binafsi kujitokeza kudhamini shindano hilo kubwa na la pekee kushirikisha wasomi wa vyuo vya kanda hiyo.

Simwita alisema wamepanga kufanya shindano lenye viwango vya kimataifa, hivyo gharama za kulifanikisha kuwa kubwa na kuomba sapoti kutoka kwa wadau.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa fainali hizo zinatarajiwa kushirikisha warembo 16 wenye elimu ya chuo kikuu, ambapo mshindi wa kwanza hadi wa tano watawakilisha vyuo vikuu Kanda ya Kaskazini katika fainali ya taifa ya Miss Utalii Tanzania Julai.

Naye mratibu wa shindano hilo, Anitha Josephat, alisema tayari warembo 12 kutoka mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro wamethibitisha kushiriki na kinachosubiriwa ni washiriki wa vyuo vya Mkoa wa Tanga, kwa ajili ya kuanza mazoezi rasmi Aprili Mosi kwenye ukumbi wa Mawingu Club.

Kila la kheri

No comments: