ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 28, 2010


Waarabu wapinga ujenzi Jerusalem
 
ujenzi mpya wapingwa Jerusalem
ujenzi mpya wapingwa Jerusalem
Jumuia inayounganisha mataifa 22 ya Kiarabu imeazimia kutounga mkono mazungumzo ya amani kati ya Israili na Palestina ikiwa mipango ya ujenzi katika Jerusalem ya mashariki itaendelea.
Haya ni maazimio mawili yaliyofikiwa kwenye kikao cha mkutano wa viongozi wa Kiarabu katika mji wa Sirte nchini Libya.
Mapema mwezi huu Jumuia hiyo iliunga mkono juhudi za Marekani katika mzozo wa Israili na Palestina.
Lakini tangu mipango ya ujenzi itangazwe katika sehemu inayoaminika chini ya sheria ya kimataifa kama inayokaliwa kimabavu mapatano yamedorora.
Katibu mkuu wa Jumuia hiyo, Amr Moussa amesema wanasubiri kuona juhudi hizo za Marekani zitaishia wapi kwa sababu hali ni tete na sharti Marekani itowe muongozo bayana kuhusu ujenzi huo.
Katibu mkuu huyo ameongezea kuwa wanatafakari kuwasilisha hoja hiyo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Mkutano huo umejitolea dola nusu bilioni za kusaidia wa Palestina wanaoishi huko Jerusalem.

No comments: