ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 29, 2010

Wasomali wapinga vitendo vya Shabab


Mamiya ya wakaazi wa mji wa Mogadishu wamefanya maandamano dhidi ya kundi la Al Shabab. Waandamanaji hao, wengi wanawake na watoto walivaa vitambaa na nguo nyeupe huku wakiwa na mabango yanayounga mkono serikali ya mpito ambayo inamiliki wilaya chache za mji.
Waandamanaji wamesema wanapinga kitendo cha kunajisi makaburi kilichofanywa na kundi la Al Qaeda pamoja na kuleta mamluki wapiganaji wa kigeni.
Mohyadin Hassan Afrah, aliyesaidia kuandaa maandamano amesema kuwa watu walikasirishwa na kitendo cha Al Shabab kuharibu makaburi ya viongozi wa madhehebu ya sufi.
Kundi la Al-Shabab linafuata imani kali ijulikanayo kama Wahabiya ya Saudi Arabia badala ya Sufi inayofuatwa na Wasomali wengi.
Halikadhalika maandamano hayo yanapinga kutumiwa kwa wapiganaji wa kigeni kwenye kundi hilo.
Mwandishi wetu anasema kuwa kuna wapiganaji kutoka Pakistan, Yemen na nchi za Afrika ya kaskazini waliomo kwenye kundi la Al Shabab

No comments: