ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 5, 2010

AWB chasema hakitalipiza kisasi

Eugene Terreblanche
Chama cha raia wa Afrika Kusini aliyeuawa - Eugene Terreblanche -aliyekuwa na msimamo mkali kuhusu ubaguzi wa rangi, kimesema hakitalipiza kisasi.
Msemaji wa chama hicho AWB, Pieter Steyn amesema hakuna mwanachama wa chama hicho atajihusisha na ghasia za aina yoyote.
Matamshi hayo yamekuja baada ya maafisa wa chama tawala cha ANC kutoa heshima zao kwa familia ya Terreblanche huku rais Jacob Zuma akitoa wito wa kuwepo na utulivu.
Polisi wamesema mauaji ya bw Terreblanche siku ya Jumamosi yametokana na mzozo juu ya malipo ya wafanyakazi.
Wafuasi wa chama cha AWB wamemtupia lawama kiongozi wa vijana wa ANC Julius Malema wakisema amehusika na mauaji hayo.

No comments: