ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 5, 2010

Ubalozi wa Marekani washambuliwa Pakistan


Smoke rises after militants attack the US consulate in Pakistan  
Watu wasiopungua saba wamekufa bada ya wanamgambo kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Peshawar, nchini Pakistan.
Kulikuwa na milipuko kadhaa katika eneo hilo la ubalozi na majengo karibu yake kuporomoka. Mapigano ya kutumia bunduki yalifuatia kati ya polisi na wanamgambo hao.
Kundi kuu la Taliban nchini Pakistan limedai kuhusika na shambulio hilo.
Shambulio hilo limekuja saa chache baada ya watu 43 kufariki katika shambulio jingine la kujitoa mhanga lililotokea karibu kilomita 80 kutoka Peshawar.
Wachunguzi wanasema shambulio hilo linahusiana na la Peshawar, ambapo polisi wameiambia BBC kuwa wanamgambo wanne na wanajeshi watatu wameuawa.

No comments: