Shirika la habari la Xinhua limesema mahakama ya China imethibitisha hukumu ya kifo ya raia wa kike wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 35 aliyetiwa hatiani kwa kufanya biashara ya dawa za kulevya.
Mwezi Julai 2009, Janice Bronwyn Linden alikutwa na hatia ya kujaribu kuingiza kilo tatu za dawa aina ya methamphetamine kupitia uwanja wa ndege wa Guangzhou mwezi Novemba 2008.
Katika hatua ya kumkatalia rufaa, mahakama kuu katika jimbo la Goangdong imesema Linden hatopewa msamaha.
Kwa sasa mahakama ya juu lazima iidhinishe uamuzi huo kabla hukumu ya Linden kutekelezwa.
No comments:
Post a Comment