ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 6, 2010

Licha ya uvumi Rooney hakufanya mazoezi


Wayne Rooney of Manchester United shows his frustration during the UEFA Champions League Group B match between Manchester United and CSKA Moscow at Old Trafford on November 3, 2009 in Manchester, England.   
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney hakufanya mazoezi na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano wa Ubingwa wa Ulaya na Bayern Munich licha ya uvumi wa uwezekano wa kurejea kucheza.
Rooney aliumia kiwiko cha mguu wa kulia wakati wa mchezo wa awali wa Ubingwa wa Ulaya dhidi ya Bayern Munich ambapo Manchester United walifungwa mabao 2-1.
Lakini Manchester United itakuwa na mlinzi wa kutumainiwa John O'Shea baada ya kuwa nje kutokanana na kuumia mguu wake wa kulia.
Bayern itakuwa na mshambuliaji wake hatari wa pembeni Arjen Robben ambaye alikosa mchezo wa awali kutokana na maumivu ya goti huku mlinzi Daniel van Buyten naye anatarajiwa kucheza.
Manchester United inahitaji bao moja tu kuweza kusonga mbele hatua ya nusu fainali.

No comments: