Raia wawili wa Afrika Kusini wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka kwa mauaji ya mzungu mwenye msimamo mkali wa masuala ya kibaguzi Eugene Terreblanche.
Polisi wamesema wakulima hao wawili, wenye umri wa miaka 28 na 15, wamekiri kumpiga mpaka kufa baada ya kuwa na mabishano juu ya kutolipwa mishahara.
Takriban wafuasi 200 wa kundi la AWB la Terreblanche lenye hadhi ya kijeshi wamekusanyika kwenye mahakama, na makundi madogomadogo kutoka jamii za watu weusi nao wapo.
Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani akiwa mjini Ventersdorp amesema polisi waliyatenganisha makundi hayo mawili baada ya kutokea fujo kidogo.
No comments:
Post a Comment