ANGALIA LIVE NEWS
Thursday, April 8, 2010
Polisi yakiri kuwapiga risasi raia
ESHI la Polisi nchini limeanzisha uchunguzi wa tukio ambalo askari wa kikosi cha Kanda Maalumu ya Kipolisi Tarime na Rorya waliwamiminia risasi raia wema wakati wa tukio la uporaji mifugo katika Kijiji cha Magoma.
Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Samson Kassala, alitoa kauli hiyo juzi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mjini hapa, akielezea mafanikio ya Operesheni Safisha iliyodumu mkoani mara kwa wiki moja.
Kassala alisema jeshi hilo linachunguza kwa makini ili kubaini chanzo cha tukio hilo kama litakuwa lilifanyika kwa uzembe ili hatua sahihi za kijeshi zichukuliwe.
“Tunakiri tukio hilo lilitushtua sana, lakini tunakiri askari wetu walihusika… napenda kuwafahamisha (waandishi) kuwa suala hilo liko katika ngazi za juu kiutawala na linashughulikiwa ipasavyo, kwa kuwa kazi yetu ni usalama wa raia,” alisema Kassala.
Usiku wa kuamkia Desemba 21 polisi walioitwa kukabiliana na wezi wa mifugo katika Kijiji cha Magoma wilayani hapa, waliwapiga risasi maeneo mbalimbali mwilini na kuwajeruhi wananchi wanne wakidhani ni wezi wa mifugo.
Wananchi hao, Sese Marigi (28), Mwita Range (19), Rhobi Manamba (25) na Piganio Marigi (26), wote wakazi wa kijiji hicho walikuwa miongoni mwa wanakijiji waliokuwa wakikabiliana na majambazi hao usiku huo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment