ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 10, 2010

Rais wa Poland afariki dunia katika ajali ya ndege

Rais Lech Kaczynski
Rais wa Poland, Lech Kaczynski, ameuwawa katika ajali ya ndege iliyotokea magharibi mwa Urusi.
Taarifa zinasema watu wasiopungua mia moja na thelathini walikuwa katika ndege hiyo na hakuna hata mmoja aliyenusurika.
Ndege hiyo aina ya Tupolev 154, ilikuwa ikisafiri kutoka Warsaw kuelekea mji wa Smolensk nchini Urusi, karibu na mpaka wa Belarus.
Ilianguka wakati ikikaribia kutua kukiwa na ukungu mkubwa.
Rais Kaczynski alikuwa akiongoza ujumbe wa Poland uliotarajiwa kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka sabini tangu kutokea kwa mauaji ya halaiki ya polisi zaidi ya elfu ishirini wa Poland.
Mauaji hayo yalifanywa na polisi maalum wa iliyokuwa Jamhuri ya Muungano wa Kisocialist ya Kisoviet, karibu na eneo la Katyn, wakati wa vita vya pili duniani.
Bw Kaczynski alichaguliwa kuwa rais mwaka wa 2005 na kabla ya hapo alihudumu kama meya wa mji wa Warsaw kwa muda wa miaka mitatu.

No comments: