| SAKATA LA KUHAMIA CCJ: Mtoto wa JK ajitosa kwa Mpendazoe | |||||||
Waandishi Wetu HATUA ya mbunge wa Kishapu Fred Mpendazoe kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama Cha Jamii (CCJ) imekipa kiwewe chama hicho tawala baada ya makada wake kutoa kauli zinazoashiria kumkebehi huku Ridhiwan Kikwete akiwatoa hofu wanachama wa chama chake. Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Mbonde, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa mikoa wa CCM, Pancras Ndejembi, mtoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan na wapigakura wa Jimbo la Kishapu jana walitoa kauli zinazotofautiana kuhusu uamuzi huo wa kihistoria. Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, Ridhiwan Kikwete alisema kujiondoa kwa Mpendazoe kumeonyesha kuwa wananchi walikuwa na mbunge wa aina yake na kuwasihi wamwache aende zake. Ridhiwan ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili mkoani Shinyanga kuhudhuria sherehe za kusimikwa kwa makamanda wa UVCCM wa wilaya, ziara ambayo imefanyika siku moja baada ya mbunge huyo kutangaza kuihama CCM na kujiunga na CCJ. |
ANGALIA LIVE NEWS
Thursday, April 1, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

1 comment:
Ujinga mtupu
Post a Comment