Uchaguzi mkuu nchini Uingereza utafanyika katika kipindi cha majuma manne yajayo.
Waziri Mkuu Gordon Brown ameafikia uwamuzi huo na raia wa nchi hiyo watapiga kura tarehe sita mwezi ujao.
Hii leo, Bw Brown atamuomba Malkia Elizabeth kulivunja bunge kabla ya kutangaza rasmi mwanzo wa kampeini za uchaguzi.
Masuala ya kodi pamoja na matumizi ya serikali wakati wa mdororo wa kiuchumi uliokumba nchi hiyo yatatawala kampeini za uchaguzi.
Chama tawala cha Labour kinajizatiti kutwaa tena uwongozi kwa mhula wa nne mtawalio ikiwa ni mara ya kwanza katika historia.
Chama kikuu cha upinzani Conservative kitahitaji kushawishi idadi kubwa ya wapiga kura ambao hawajakata kauli ya kuunga upande wowote kwa miongo sita ili kujipatia viti vingi katika bunge.
No comments:
Post a Comment