Rais Barack Obama anatarajiwa kutangaza mkakati mpya wa ulinzi utakaopunguza vyanzo vitakavyoweza kuchochea Marekani kutumia zana zake za nuklia.Mkakati huo utazuia Marekani kujibu mashambulizi yoyote ya kemikali au zana nzito dhidi yake kwa kutumia silaha za nuklia.
Aidha Obama atatangaza kuwa Marekani haitaweza tena kutumia zana za nuklia dhidi ya nchi zisizotumia zana hizo au nchi zinazotii azimio linalopinga kutengenezwa kwa zana za nuklia.
Hata hivyo ametaja Iran na Korea Kusini kama miongoni mwa nchi zinazokiuka azimio hilo akisema Marekani itajitahadharisha nazo.
Rais Obama amesisitiza kuwa Iran ipo mbioni kuunda zana za nuklia na hivyo angependa kuona Umoja wa Mataifa ukiiwekea nchi hio vikwazo, katika wiki chache zijazo.
No comments:
Post a Comment