ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 10, 2010


Wasomali 66 wapigwa changa la macho kweupeee!

Raia 66 wenye asili ya kisomali waliokuwa safarini kwenda Msumbiji wamedakwa wilayani Kilwa, mkoani Lindi baada ya kuingizwa mjini.

Wasomali hao walitelekezwa ktk eneo la bandari ya Songo-Mnara wilayani humo....baada ya kukodi jahazi jijini dsm wakitaka wapelekwe msumbiji.

Habari inaelezwa kuwa kutokana na ugeni wao wa kutokujua sehemu wanayokwenda,baada ya kufika bandari hiyo ya Songo-Mnara wenye majahazi waliwaeleza kuwa wameshafika kule walikokusudiwa kupelekwa..yaani Msumbiji.

Wasomali hao akiwemo mwanamke mmoja pamoja na watoto wao baada ya kushuka kwenye majahazi hayo na baada ya wananchi kuona kundi hilo la watu wasioeleweka walipiga simu polisi na walifika mara moja na kukamatwa ambapo bado wanashikiliwa hadi hivi sasa.

Imeelezwa kuwa kutokana na wingi wao imebidi idara inayohusika kuwahifadhi kwa kuwapatia madarasa mawili katika Shule moja ya msingi ya mjini humo wakisubiria taratibu nyigine za kisheria.


No comments: