ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 30, 2010

July 4th Weekend Minnesota


 huu ndio miji mapacha karibu na  Minneapolis-St. Paul International Airport ambapo July 4th Weekend patakua hapatoshi mambo yanaanza July 1-4

Mtanzania ahusishwa jaribio la mauaji ya jenerali Nyamwasa

OBURG, Afrika Kusini
south africaMTANZANIA mmoja ni miongoni mwa watu waliofikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini kwa tuhuma za kuhusika katika jaribio la mauaji ya mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda, Luteni Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa mjini Johannesburg Juni 19.

Waendesha mashtaka nchini humo pia waliwafikisha mahakamani watu wengine raia wa Somalia na Msumbiji kwa tuhuma za jaribio hilo la mauaji, ambapo Nyamwasa alinusurika baada ya kupigwa risasi tumboni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari Afrika Kusini, ilielezwa mahakamani hapo kwamba watuhumiwa hao pia wana historia ya uhalifu na kukutwa na vifaa vilivyoibwa.

Baada ya kusomewa mashtaka dhidi yao, watuhumiwa hao kwa pamoja walirejeshwa mahabusu baada ya kesi yao kuahirishwa hadi mwezi ujao ili kuruhusu uchunguzi kuhusu uhalali wao kuwepo nchini humo utakapokamilika.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani baada ya polisi kuwaachia huru watuhumiwa wengine wawili wiki iliyopita, ambao pia walikamatwa kwa tuhuma za kuhusishwa na jaribio hilo la mauaji.

Luteni Jenerali Nyamwasa, kiongozi wa zamani wa jeshi la Rwanda aliyekimbilia uhamishoni mwezi Februari mwaka huu, alinusurika katika jaribio la kumuua Jumamosi Juni 19 alipokuwa akitoka kufanya manunuzi ya vifa vya nyuimabni akiwa na mkewe.

Nyamwasa alikimbilia nchini Afrika Kusini baada ya kutofautiana na mshirika wake wa muda mrefu, Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya kumtuhumu kwamba amekuwa akijihusisha na rushwa.

Mke wa Luteni Jenerali Nyamwasa, Rosette amekuwa akiilaumu serikali ya Rwanda akidai kwamba inahusika na jaribio hilo ambapo mtu mwenye silaha alimpiga risasi tumboni kisha kutoweka bila kuchukua kitu chochote.

Tuhuma hizo zimekanushwa na serikali ya Rwanda ambayo imekuwa ikimtuhumu Nyamwasa kwa kuhusika na milipuko ya mabomu iliyotokea mjini Kigali mwezi Februari na kuitaka serikali ya Afrika Kusini imrejeshe pamoja na Kanali Patrick Karegeya ambao kwa pamoja walikimbia nchini humo.

BBC

Tanzania yawatuliza wanaopinga uuzaji meno ya tembo



Meno ya Tembo yakiwa yamehifadhiwa
Na mwandishi wetu, Dodoma
MAZUNGUMZO ya kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda yamefanyika, ili kuzifanya nchi hizo zisiweke pingamizi wakati Tanzania itakapopeleka tena mswada wa kuomba kuruhusiwa kuuza sehemu yake ya meno ya ndovu .

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, ambaye alisema chini ya mazungumzo hayo, serikali ilizieleza nchi hizo nia yake ya kutaka kuuza sehemu ya pembe za ndovu.

Alisema kwa msingi huo, serikali haitegemei tena kama kutakuwa na kikwazo kutoka katika nchi hizo wakati mswada huo utakapowasilishwa tena ili kuomba ruhusa ya kuuza pembe hizo.


Maige alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi wananchama wa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti biashara ya kimataifa wa wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka (Cites), uliosainiwa  mwaka 1973 na kuanza kutekelezwa mwaka 1975.

Alisema kwa upande wake, Tanzania iliridhia mkataba huo mwaka 1980.

Alisema kutokana ongezeko la ujangili dhidi ya tembo na biashara ya meno ya wanyama hao, mwaka 1988, Tanzania ilisimamisha biashara ya meno ya tembo, jambo linaloonyesha nchini ilikuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za Cites.

Kwa mujibu wa Naibu waziri, tangu wakati huo meno ya tembo hapa nchini yamekuwa yakihifadhiwa katika maghala ya kuhifadhia nyara za serikali bila kufanyiwa biashara.


Alisema kuongezeka kwa idadi ya tembo hapa nchini, kutoka 55, 000 mwaka 1989 hadi kufikia 110,000 mwaka 2009 pia kumesababisha kuongezeka kwa meno ya tembo kwenye ghala.

"Lakini pia hali hiyo imesababisha kuongezeka kwa gharama za kutunza meno hayo. Kwa hiyo mwaka 2010 Tanzania iliamua kuwasilisha kwa Sektrerieti ya Cites muswada wa kuuza meno ya tembo ili ujadiliwe katika mkutano mkuu wa 15 wa nchi wanachama," alisema.

Alisema uamuzi wa kuwasilisha muswada  kama huo ni wa kawaida ingawa hata hivyo kuna propaganda dhidi ya Tanzania.

Alisema propaganda hizo  zilifanywa  na mashirika mbalimbali ya kimataifa yasiyo ya kiserikali na baadhi ya nchi za Afrika zikiwemo nchi jirani.


Alisema kwa jumla,  propaganda hizo ziliathiri kusudio la Tanzania kwa sababu zilitoa picha potofu.

Maige alisema baadhi ya wapotoshai hao walidai kuwa fedha ambazo zingepatikana kwa kuuza meneno hayo zingetumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na si kwa uhifadhi wa tembo.


Maige alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kongwa,Job Nduai aliyetaka kauli ya serikali kuhusu hatma ya meno ya ndovu yaliyohifadhiwa ghalani

Nigeria 'suspends' football team


Nigerian fans have been underwhelmed by their team's performances in South Africa [Reuters

Nigeria's president has suspended the national football team from international competition for two years following their poor performance at the Fifa World Cup


HOTUBA YA SHUKRANI YA MAALIM SEIF

HOTUBA YA SHUKRANI YA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CUF, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU MAALUM WA TAIFA WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
LANDMARK HOTEL, DAR ES SALAAM – 27 JUNI, 2010
Mheshimiwa Mwenyekiti wa CUF Taifa,
Mheshimiwa Makamo Mwenyekiti,
Waheshimiwa Manaibu Katibu Mkuu,
Waheshimiwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa,
Waheshimiwa Wageni wetu waalikwa,
Mabibi na Mabwana,
Kwa mara nyengine tena, namshukuru kwa namna ya pekee Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia afya njema na uzima hadi tukaweza kukamilisha kazi kubwa iliyotuleta hapa ya kuwachagua Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama chetu.
Nawashukuru nyinyi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa pia kwa imani yenu kubwa mliyonipa ya kunichagua kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama chetu. Imani yenu kwangu naithamini sana. Naithamini sana kwa sababu ni dalili ya mapenzi makubwa kwangu ambayo naamini yametokana na jinsi nilivyoweza kufanya kazi nanyi kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja katika hali ya uaminifu na kujituma wakati natekeleza majukumu mliyonipa. Siipati kauli nyengine ya kueleza shukrani zangu zaidi ya kuwaambia Ahsanteni sana.
Natumia fursa hii pia kumpongeza sana Mheshimiwa Prof. Ibrahim Lipumba kwa kuchaguliwa kwake kwa kura nyingi na nyinyi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha CUF. Nimemjua Prof. Lipumba kwa miaka mingi sasa na pia nimefanya kazi naye kwa ukaribu katika kipindi cha takriban miaka 15 sasa, kwanza akiwa Mgombea wetu mwaka 1995 na baadaye kama Mwenyekiti wangu kuanzia 1999 hadi sasa. Sina shaka wala wasiwasi kwamba Prof. Lipumba ni ndiye mtu anayefaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inahitaji kiongozi atakayejenga uchumi imara utakaotoa ajira na neema kwa wote kwa kuwainua Watanzania masikini na kuwongezea kipato chao mwaka hadi mwaka badala ya kujenga uchumi legelege unaowanufaisha wachache na kuendelea kuwafukarisha walio wengi. Hongera sana Prof. Lipumba na naamini utaipeperusha vyema bendera ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao naamini utaleta mabadiliko makubwa kwa Chama chetu.
Nampongeza pia Mheshimiwa Juma Duni Haji kwa kuteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa kuwa Mgombea Mwenza wa Prof. Lipumba. Naamini kutokana na uzoefu na umahiri wake wa kazi, atashirikiana vyema na Mgombe Urais kuwadhihirishia Watanzania kuwa CUF ina timu imara ya kuleta mabadiliko yanayohitajiwa sana na Watanzania.
Waheshimiwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu, nimesema kwamba naithamini sana imani mliyoionyesha kwangu. Mmenipa imani kama hii huko nyuma lakini mara hii mmefanya hivyo katika mazingira tofauti ya kisiasa. Maridhiano ya Wazanzibari yaliyoanzishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Amani Abeid Karume, na mimi tarehe 5 Novemba, 2009 yamebadilisha kabisa sura na mahusiano ya kisiasa baina ya wananchi wa Zanzibar na hasa baina ya wafuasi wa vyama vyetu viwili, CUF na CCM.
Kuna uwezekano wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa mwaka huu kufanyika katika mazingira ya uhuru, haki na uwazi. Rais Karume amekuwa akisisitiza mara kadhaa kwamba hilo ndilo lengo lake na la Serikali yake kuona uchaguzi wa mwaka huu unakuwa huru na wa haki ambao utawafanya washindani wote waridhike na kusiwepo na malalamiko ukiondoa yale ya kibinadamu. Ni imani yangu kwamba Rais Karume ataisimamia kauli yake hiyo kwa vitendo. Hivyo basi, naamini katika mazingira hayo na tukishirikiana wanachama wote wa CUF kufanya kampeni kabambe, za kisasa na za kistaarabu hapana sababu kwa nini tusishinde uchaguzi huu na kuiongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Lakini uchaguzi wa mwaka huu pia utakuwa ni tofauti kwa sababu matokeo yake yatapelekea Zanzibar kuanzisha muundo mpya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Najua kuwa hili litategemea maamuzi ya wananchi kupitia kura ya maoni itakayofanyika Zanzibar tarehe 31 Julai, 2010, lakini mimi naamini kabisa Wazanzibari wamechoshwa na hali ya magomvi, uhasama na chuki iliyodumu kwa takriban miaka 50 sasa, na hivyo basi naamini kwa umoja wao na kwa asilimia kubwa sana watapiga kura ya NDIO kuridhia muundo huo mpya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kwa hakika, nataka kutumia fursa hii kutoa wito hasa kwa wananchi wote wa Zanzibar, walio CUF, CCM, wa vyama vyengine na wasio wafuasi wa chama chochote, wote kwa ujumla wao wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 31 Julai, na wapige kura ya NDIO ili kwa pamoja tuijenge Zanzibar Mpya; Zanzibar shirikishi na siyo Zanzibar tenganishi; Zanzibar itakayokuwa na neema kwa wote.
Waheshimiwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu, mmenichagua niinue juu bendera ya CUF kwa madhumuni ya kuwaomba Wazanzibari ridhaa yao ili niiongoze Zanzibar Mpya tuliyoazimia kuijenga. Naamini tutafanikiwa. Lakini nilitaka basi niyataje japo kwa ufupi tu mambo kumi (10) ambayo yatakuwa ndiyo msingi wa maongozi yangu katika kipindi cha miaka mitano ijayo, na ambayo yatakuwa ndiyo pia msingi wa Ilani ya Uchaguzi ya CUF kwa upande wa Zanzibar. Mambo hayo kumi (10) ni haya yafuatayo:
Kuyaendeleza Maridhiano ya Kisiasa tuliyoyaasisi mimi na Rais Amani Karume yakiwa ndiyo njia sahihi ya kujenga umoja wa kweli miongoni mwa Wazanzibari na kuendeleza amani na utulivu uliopo kwa kufuata misingi ya ukweli na mapatano.
Kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kwa mujibu wa makubaliano ya CUF na CCM yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo ya Bagamoyo na ambayo yaliridhiwa na vyama vyetu viwili kupitia vikao vya juu vya maamuzi vya vyama vyetu.
Kuuimarisha Muungano wetu kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kuendeleza mazungumzo yenye nia ya kweli ya kuyapatia ufumbuzi wa dhati matatizo yanayoukabili chini ya misingi ya haki, usawa na kuheshimiana baina ya pande mbili zinazounda Muungano huu.
Kujenga uchumi imara kwa kuzingatia mfumo wa soko huria unaotoa fursa ya ushiriki kwa wananchi wote na ambao unaratibiwa vyema na Serikali ili kuhakikisha kuwa wananchi wetu wote wanafaidika na fursa hizo na kunyanyua hali zao za maisha katika hali ya neema na tija kwa wote. Sekta za Kilimo, Utalii, Biashara, Viwanda na Uvuvi zitapewa kipaumbele katika ujenzi wa uchumi wa kisasa kwa Zanzibar Mpya.
Kuimarisha nidhamu ya utendaji kazi Serikalini na ubora wa huduma zinazotolewa na utumishi wa umma kwa kusimamia ipsavayo kanuni za kazi, kuwapatia mafunzo ya kazi kadiri inavyowezekana na kuwaongezea mishahara wafanyakazi wetu ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na kuwa mfano kwa umma.
Kwa kufuata mfumo wa uchumi wa soko huria, kuirudisha Zanzibar katika hadhi yake ya kituo kikuu cha biashara na huduma katika eneo lote la Afrika Mashariki kwa kutekeleza sera zitakazoweka mazingira mazuri na yanayovutia ya kufanyia biashara na kuleta uwekezaji mkubwa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuimarisha bandari zetu na viwanja vya ndege vitakavyoweza kutuunganisha na nchi za nje na nchi jirani.
Kukiendeleza kilimo na kukirejeshea hadhi yake kama moja ya njia kuu za uchumi inayotegemewa na wananchi wetu walio wengi hasa wa vijijini. Mkazo utawekwa katika kilimo cha viungo na mboga mboga ili tuendelee kutumia vyema soko linaloweza kupatikana kutokana na jina maarufu la Zanzibar kama visiwa vya viungo.
Kuweka msukumo maalum katika kuinua viwango vya elimu katika skuli zetu za msingi, sekondari hadi vyuo vikuu ili Zanzibar iwe ndiyo kituo kikuu cha elimu na mafunzo stadi katika eneo lote la Afrika Mashariki. Mkazo utawekwa katika kusomesha walimu kwa viwango vya kimataifa, kuwapatia maslahi bora ili kuirejeshea hadhi fani na kazi ya ualimu, kuboresha mazingira ya skuli zetu na taasisi za elimu ya juu kwa kuzipatia huduma zote muhimu zinazohitajika kwa ukuzaji wa elimu, kujenga na kuimarisha maabara za kisasa, na kupunguza ukubwa wa madarasa na idadi ya wanafunzi ili walimu waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuipitia upya mitaala yetu ili iendane na mahitaji ya Zanzibar ya leo kulingana na sera za uchumi tutakazozifuata.
Kuinua na kuimarisha huduma za afya katika hospitali, zahanati na vituo vya afya kwa kuweka vifaa vya kisasa vya matibabu, kuvipatia madawa yote muhimu, kusomesha na kuajiri madaktari na wauguzi wapya, kuboresha maslahi ya madaktari na wauguzi, kuwawekea mazingira bora ya kufanyia kazi na kuhakikisha usafi katika sehemu hizo.
Kurejesha maadili mema ya Wazanzibari kwa kuhuisha mila, silka na utamaduni wetu na kuwarejeshea Wazanzibari hadhi na fahari yao iliyotokana na mila, silka na utamaduni huo. Katika kurejesha maadili hayo, Serikali nitakayoiongoza itapambana vikali na uingizaji na utumiaji wa madawa ya kulevya ambao umekuwa ukiongezeka kwa kasi visiwani Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa sheria zinatekelezwa na kusimamiwa ipasavyo ili kudhibiti uingizaji na pia kuanzisha na kuviendeleza vituo vya kuwasaidia waathirika wa madawa hayo ya kulevya ili waache utumiaji huo.
Ndugu zangu, wajumbe wa Mkutano Mkuu, haya niliyoyaeleza hapa siyo mambo pekee yatakayotekelezwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa nitakayoiongoza. Haya ni mambo nitakayoyapa umuhimu wa kipekee lakini yatajenga msingi wa kuyaendeleza mambo mengine katika sekta na nyanja zote za maisha. Haya na mengine yataelezwa na kufafanuliwa kwa upana zaidi katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama chetu tutakayoizindua wakati wa kampeni ukifika.
Kwa ufupi, tunakusudia kujenga Zanzibar mpya ili ifikie kule ambapo Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, alitaka kila Mzanzibari afikie na kujinasibu nako ikiwa ndiyo malengo ya Uhuru waliokuwa wakiupigania wazee wetu hao. Katika Ilani ya Uchaguzi ya ASP ya mwaka 1961, Mzee Karume aliieleza vyema Zanzibar hiyo kwa maneno yafuatayo:
“UHURU ndio msingi wa siasa ya chama chetu. Unachanganya bila ya shaka kumalizika kwa Serikali ya Kikoloni na mwisho wa utawala wa nje. Kadhalika UHURU unakusanya ukunjufu kutokana na ujinga na haja zisizokwisha. UHURU wa kuwa na pato la kumwezesha mtu kuyatekeleza yaliyombidi, kustarehe na kuwa mtu, uhuru wa kuishi kama watu katika nchi yetu.
Huu ndio UHURU ambao daima tukiutaka, huu ndio UHURU ambao daima twaupigania, huu ndio UHURU ambao tumejitolea kuutumikia na siku zote tutautumikia kwa nguvu zetu zote na kwa uwezo wetu wote.
Tunadhani kuwa kila mmoja wetu katika visiwa hivi aendelee mbele kwa mujibu wa uwezo wake, jambo ambalo ni gumu lakini kabisa si jambo lisilowezekana. Na iwapo wewe Kilillahi huyapingi haya tuliyoazimia na wewe mwenyewe ndiye uwezaye kujua, basi tafadhali karibu uungane nasi twende pamoja na kuutia mkononi huu UHURU.”
Wazee wetu waliupigania na kuutia mkono UHURU huu. Sasa ni wajibu wetu sisi kuendeleza pale walipotuachia ili tuyafikie kweli malengo ya UHURU huo walioupigania kama alivyoyaeleza Marehemu Mzee Karume. Naamini tukiyasimamia na kuyatekeleza vyema mambo haya kumi (10) niliyoyataja hapa, basi tutaweza kuyafikia malengo hayo.
Ahsanteni sana.
Dar es Salaam
27 Juni, 2010
Image
Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwa kwenye msururu mferu wa kuingia kwenye ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Manispaa ya Kinondoni kulipia kodi za majengo, jana. Mwisho wa zoezi hilo ulikuwa ni jana. (Picha na Yusuf Badi).

Mzalendo Pub....Kiwanja cha wajanja


Elizabeth Barden kutoka DENMARK ndani ya Mzalendo Pub

ndani YA MZALENDO PUB kila Jumamosi
yaani ni raha tuu


Daudi kulia akia na Dj Venture huku sis hataki kukosa u-kodak moment ndani ya Mzalendo Pub

JULY 4TH,WEEKEND & DICOTA CONVENTION 2010 JULY 1-4,MINNESOTA



 2 July ijumaa na July 4 Jumapili Dj Luke kutoka DC,atakupa ile kitu roho inapenda ndani ya
MARRIOTT HOTEL,DOWNTOWN MPLS,
30 SOUTH,7TH STREET,
MPLS,MN,55402



Jumamosi ni Rumba ndani ya Boti na Dj Luke,kukusuuza na burudani
Address,From 7:30pm-1:00am
525 SOUTH MAIN STREET,
STILL WATER,MN,55408
Jumapili ni ULTIMATE SOCCER BONANZA,Stars United,Houston(Serengeti Boyz),Uganda(The Crane) naWenyeji Minnesota Stars na kama wewe ni mpenzi wa BBQ usisahau TOOTHPICK,Nyama ni za kumwaga,Address,From 2:00pm-8:00pm,
DRIFTWOOD PARK,
2705 5TH STREET,NW,
NEW BRIGHTON,MN
Kikosi cha Minneota
Kikosi cha Houston

Kikosi cha Stars
Uganda(The Cranes)


Je unaukumbuka Mshumaa huu

Miss & Mr East Africa UK Rehersal 2010

Tuesday, June 29, 2010

Should Naomi Campbell Ditch the Weaves for Good?


Being a supermodel is not as easy as it looks.
Image
Wakazi wa eneo la Mgulani barabara ya Chang’ombe Dar es Salaam wakiwa katika mstari wa kusajili simu zao kama walivyokutwa jana. Mwisho wa zoezi hilo ni leo. (Picha na Yusuf Badi)

BMW 525 I INAUZWA BEI POA

Reliable and dependable: Used BMW, year 1995, Automatic, mileage 200k

Price: Best Offer -still in very good condition,Two Owners

For more info: Call 703 624 2409


Oprah Winfrey, atisha kwa utajiri

Oprah Winfrey
Mtangazaji wa televisheni Marekani Oprah Winfrey ametajwa kuwa mtu mwenye mvuto na utajiri mkubwa duniani kupitia jarida la Forbes.
Winfrey amempiku muigizaji wa filamu Angelina Jolie kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya watu 100 mashuhuri kwa mwaka katika jarida la Forbes.
Nafasi hizo hupangwa kutokana na mapato ya mtu na kiwango anachoonekana kwenye vyombo vya habari.
Muimbaji Beyonce, amechukua nafasi ya pili, huku mkurugenzi wa filamu James Cameron akiingia tena kwenye chati na kuchukua nafasi ya tatu kufuatia mafanikio yake ya filamu ya Avatar.
Lady Gaga amepanda katika nafasi mpya ya orodha hizo akiwa nafasi ya nne.
Kama ilivyo kwa Beyonce, mapato yake na taarifa za maisha yake kwa ufupi zimeongezeka katika miaka 12 iliyopita kutokana na ziara zake duniani na mikataba mbalimbali.
Jolie, wakati huo huo, ameteleza kutoka nafasi ya juu hadi kufikia nafasi ya 18.
Nyota wa gofu aliyezingirwa na matatizo mengi Tiger Woods ni nyota pekee wa michezo kuwa katika 10 bora.
Simon Cowell
Simon Cowell
Britney Spears amekuwa wa sita, ikufuatiwa na U2 kwenye nafasi ya saba, wakiwa wamerudi katika 100 bora.

Sandra Bullock, aliyeshinda tuzo ya Oscar mwaka huu ya muigizaji bora wa kike, amepanda chati kwa kasi kutoka nafasi ya 92 hadi kufikia ya nane.
Johnny Depp naye amerudi kwenye chati katika nafasi ya tisa.
Kigogo wa muziki Simon Cowell ameongoza kwa upande wa Uingereza, kwa kupanda nafasi 14 hadi kufikia nambari 11.
Lakini Clodplay imeshuka kwa nafasi 20 na kuwa ya 35 katika mwaka ambao bendi hiyo imepumzika kufanya ziara na kuamua kurejea studio.
Nyota wa Harry Potter Daniel Radcliffe ameshika nafasi ya 82.
Umaarufu wa mfululizo wa Twilight ulionekana kwa kuwepo muigizaji wa kike Kirsten Stewart akiwa nafasi ya 66 na Robert Pattinson nafasi ya 50, wote wakiwa kwenye orodha hiyo kwa mara ya kwanza.
Mwaka huu, Forbes iliongeza kigezo cha mtu maarufu kuwepo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook au Twitter, pamoja na mapato na kiwango cha kuonekana kupitia vyombo vya habari.

Pata kideo ya Mitumba inakotoka mpaka kufika Tanzania

Monday, June 28, 2010

AROBAINI YA NJITI,JULY 3



FAMILIA YA ABDELLE ABILAHI INAKUTAARIFU AROBANI YA MDOGO WAKE KIPENZI,MAREHEMU YUSUF MOHAMED ABILAHI KWA JINA MAARUFU NJITI ITAKAYOFANYIKA JULY 3 SAA TISA(3PM) LANGLEY PARK,

2929 EDGEWOOD RD,
KENSINGTON,MD,20895

KWA MAELEZO NA MAELEKEZO ZAIDI,202 560 4420 ABDELLE

Kobe Bryant Visits Football Centre In Soweto - 2010 FIFA World Cup

Basketball player Kobe Bryant visits a football centre during the 2010 FIFA World Cup South Africa on June 27, 2010 in Soweto, South Africa.
Basketball player Kobe Bryant visits a football centre during the 2010 FIFA World Cup South Africa on June 27, 2010 in Soweto, South Africa.
Basketball player Kobe Bryant visits a football centre during the 2010 FIFA World Cup South Africa on June 27, 2010 in Soweto, South Africa.
Basketball player Kobe Bryant visits a football centre during the 2010 FIFA World Cup South Africa on June 27, 2010 in Soweto, South Africa.
Basketball player Kobe Bryant visits a football centre during the 2010 FIFA World Cup South Africa on June 27, 2010 in Soweto, South Africa.
Basketball player Kobe Bryant visits a football centre during the 2010 FIFA World Cup South Africa on June 27, 2010 in Soweto, South Africa.
Basketball player Kobe Bryant visits a football centre during the 2010 FIFA World Cup South Africa on June 27, 2010 in Soweto, South Africa.
Basketball player Kobe Bryant visits a football centre during the 2010 FIFA World Cup South Africa on June 27, 2010 in Soweto, South Africa.

Michael Jackson's Jeweled Glove Sells for $190K


MJ memorabilia is not cheap. Two hundred items sold at auction last week brought in a total of about $1 million.

BET Awards June 27 2010

Actress Kim Coles arrives at the 2010 BET Awards held at the Shrine Auditorium on June 27, 2010 in Los Angeles, California.
Actress Kim Coles arrives at the 2010 BET Awards held at the Shrine Auditorium on June 27, 2010 in Los Angeles, California.
Actress Tatyana Ali arrives at the 2010 BET Awards held at the Shrine Auditorium on June 27, 2010 in Los Angeles, California.
Actress Tatyana Ali arrives at the 2010 BET Awards held at the Shrine Auditorium on June 27, 2010 in Los Angeles, California.
Nick Cannon arrives at the 2010 BET Awards held at the Shrine Auditorium on June 27, 2010 in Los Angeles, California.
Nick Cannon arrives at the 2010 BET Awards held at the Shrine Auditorium on June 27, 2010 in Los Angeles, California.
Actor Tyler James Williams arrives at the 2010 BET Awards held at the Shrine Auditorium on June 27, 2010 in Los Angeles, California.
Actor Tyler James Williams arrives at the 2010 BET Awards held at the Shrine Auditorium on June 27, 2010 in Los Angeles, California.
Kwa pcha zaidi BOFYA HAPA

Minnesota hiyoooo,July 4th Weekend




Kikosi cha Minneota
Kikosi cha Houston

Kikosi cha Stars
Uganda(The Crane)
Mambo yote july 4th weekend ni Minnesota,pati ya Boti,kata tiketi mapema usije ukajutia,kama unakumbukumbu ya zile pati za OHIO,wakati wa mermorial weekend,au DC,wakati wa labor day weekend,basi hautasita kukwaa pipa na kuelekea miji mapacha,kama upo jirani aaah ndugu yangu usisite kuchoma gari moto,safari hii wanakuletea BONGO R&B SINGER,MARLOW,KUTOKA TANZANIA
mambo yanaanzia tarehe 2 July ijumaa,kwa Marlow kufanya vitu vyake akishirikiana na Dj Luke kutoka DC,address,
MARRIOTT HOTEL,DOWNTOWN MPLS,
30 SOUTH,7TH STREET,
MPLS,MN,55402
Jumamosi ni Rumba ndani ya Boti,Marlow kumalizia kiu yako akishirikiana na Dj Luke,
Address,From 7:30pm-1:00am
525 SOUTH MAIN STREET,
STILL WATER,MN,55408
Jumapili ni ULTIMATE SOCCER BONANZA,Stars United,Houston(Serengeti Boyz),Uganda(The Crane) naWenyeji Minnesota Stars na kama wewe ni mpenzi wa BBQ usisahau TOOTHPICK,Nyama ni za kumwaga,Address,From 2:00pm-8:00pm,
DRIFTWOOD PARK,
2705 5TH STREET,NW,
NEW BRIGHTON,MN,
Baadae ni Farewell Party From 10:30pm-3:00am,
MARRIOTT HOTEL,DOWNTOWN MPLS,
30 SOUTH 7TH STREET,
MPLS,MN,55402
kuikosa pati boti  hii ni KOSA LA JINAI!!!