
Kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya nchini kilicho chini ya Kamishna wa Polisi Godfrey Nzoa kimewakamata raia wawili wa kigeni katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Cocaine ndani ya mabegi yao huku wakisema kuwa wao ni maafisa Balozi.
Katika taarifa yake Kwa vyombo vya habari kamishna Nzoa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Diaka Brama Kara (52) raia wa Guniea, Conakry na Abubakar Ndijane (50) raia wa Liberia, Monrovia.

Kamishna Nzoa akiongea na wanahabari kuhusiana na tukio hilo leo katika makao makuu ya jeshi la polisi.

Kamishna Nzoa akionyesha wanahabari mabegi yalitotumiwa na watuhumiwa kubebea madawa hayo.

Afisa upelelezi kitengo cha madawa ya kulevya, Koplo Wamba Msafiri, akionesha baadhi ya madawa aina ya Cocaine.
Picha: Haruni Sanchawa
No comments:
Post a Comment