ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 25, 2010

Uwanja wa Simba kukarabatiwa wiki ijayo

Mwenyekiti wa Simba Aden Rage (kushoto) akizungumza na mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya Simba Joseph Itang’are.
Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umemwagiza meneja wa uwanja wa Kinesi uliopo Urafiki jijini Dar es Salaam, kuorodhesha bajeti ya vifaa vitakayotumika kwa ajili ya ukarabati wa uwanja wa Kinesi ambao utatumiwa kwa mazoezi kwa muda na timu hiyo.
Ukarabati huo utakuwa ukifanyika huku uongozi wa timu hiyo, ukiendelea kufuatilia viwanja vya Bunju na Ilala ambavyo pia ni vya Simba. Ukarabati utaanza rasmi wiki ijayo ambapo kutakuwa pia na gym ambayo itakuwa na kifaa cha kupozea hewa ‘Air Condition’ na mabafu.

katibu mkuu wa uwanja wa kinesi Lincoln Joseph (kushoto0 akiwa na mwenyekiti wa klabu ya Simba Aden Rage pamoja mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba ambaye pia ni mmiliki wa uwanja wa kinesi wakitafakari jambo juu ya maboresho ya uwanja
Picha: Leah Kwenda

No comments: