ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 20, 2010

Msiba wamzuia Bilali kutangaza Urais Z'bar

Saturday, 19 June 2010 21:29
 Salma Said, Zanzibar
KIU ya wananchi ya kutaka kusikiliza maoni ya mwanasiasa maarufu visiwani Zanzibar , Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilali imezimika ghafla baada ya jana kuahirisha mkutano wake na waandishi wa habari kufuatia kifo cha kaka yake Bilal Gharib Bila

Tayari macho na masikio ya watanzania wafuatiliaji wa duru za kisiasa yalikuwa yameelekezwa visiwani humo, kusikia kigogo huyo ambaye baadhi ya tafiti zimemuonyesha bado ana nguvu, angesema nini katika kipindi hiki ambacho joto la uchaguzi hasa nafasi ya urais likiwa juu visiwani humo.

Ratiba ya CCM kutoka Ofisi Kuu ya Kisiwandui iliyotolewa juzi, tayari imeweka bayana vigogo watakaochukua fomu za kuomba ridhaa ya chama hicho kwa jili ya urais wa visiwa hivyo, miongoni mwao yumo Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein.

Hata hivyo, mbio hizo ndefu za kuwania nafasi hiyo ya kuchaguliwa ndani ya chama ilianza kwa dosari kwa Dk Bilali baada ya kusambazwa taarifa kwa ujumbe mfupi wa simu (SMS) juu ya kifo hicho cha kaka wa waziri kiongozi huyo mstaafu.
“Innah lillah wainnah ilayhi rajiun. Tunasikitika kukuarifu kuhusu kuahirishwa kwa tukio la press conference ya leo (jana) Zanzibar Ocean View kutokana na kifo cha kaka yake Dk. Bilal Mohammed Bilal hadi hapo itakapotolewa taarifa nyengine. Tunasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza, tafadhali muarifu na mwenzio” unasomeka ujumbe huo ambao umetumwa nyakati za usiku.
Hata hivyo, tangazo hilo la kifo pia lilitangazwa kupitia Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) asubuhi katika kipindi cha matangazo ya vifo, marehemu katika uhai wake aliwahi kushika nyadhifa kadhaa ikiwemo ile ya kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Watu Wazima Zanzibar maziko yake yamefanyika jana laasiri kijijini kwao Mwera.
Waziri kiongozi mstaafu alipanga kuzungumza na waandishi wa habari kutangaza nia yake ya kuchukua fomu siku ya jumatatu majira ya saa mchana ambapo akitanguliwa na waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha.

No comments: