Mtoto awahenyesha Kaka, Robinho na Kikwete
Mtoto kati ya wale waliotoka na wachezaji wa Brazil kabla ya mechi dhidi ya Taifa Stars aliwapa wakati mgumu nyota Luis Fabiano, Kaka na Robinho kutokana kutotulia. Hali hiyo iliwafanya wachezaji hao kushindwa hata kuimba wimbo wao wa taifa, kutokana na kulazimika kufanya kazi ya ziada kumtuliza kinda huyo mwenye vituko.
Wakati mwingine wakilazimika kumbeba na hata kuita watoto wengine wampoze, lakini wapi, badala yake aliwapiga mateke wenzake hao ambao walisalimu amri na kuwaacha Fabiano, Kaka na Robinho waendelee naye.Wakati Rais Jakaya Kikwete amemfikia, kinda huyo aligoma kutoa mkono wake na kuiingiza ndani ya jezi, hadi Fabiano na Kaka walipomvisha jezi yake vizuri ndipo akakubali kumsalimia Rais.
PICHA ZOTE NA SALEH ALLY
No comments:
Post a Comment