Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (wa pili kushoto) akipokea hundi ya Sh 100 milioni jijini Dar es salaam kutoka kwa Mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa CCM, Mustafa Jaffar Sabodo huku katibu mkuu wa chama hicho Dr Willibrod Slaa akishuhudi
Geofrey Nyang’oro
VYAMA vya upinzani sasa vinaweza kuwa vimepata matumaini mapya ya vyanzo vya fedha baada ya mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa CCM, Mustapha Sabodo kutoa mchango wa Sh100 milioni kwa Chadema.Sabodo, ambaye anaendesha biashara za aina mbalimbali, pia atakuwa tayari kukichangia chama hicho fedha wakati mwingine wowote, kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo.
Mchango huo ambao umewekwa bayana unafungua ukurasa mpya kwa vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa vikisumbuliwa na ukata wa fedha kutokana na kutokuwa na vyanzo vya fedha.
Vingi vinategemea ruzuku, lakini mgao wao ni mdogo kutokana na kuingiza wabunge wachache bungeni na kutopata kura za kutosha kwenye kinyang'anyiro cha urais.
Wakati CCM ikifaidi ruzuku kutokana na kufanya vizuri kwenye uchaguzi, wafanyabiashara wamekuwa wakimimina misaada na michango yao kwa chama hicho tawala, wengi wakionekana kuwa na hofu ya kuchangia kwenye vyama vya upinzani huku wale wanaothubutu wakifanya hivyo kwa usiri mkubwa

KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA.
No comments:
Post a Comment