Na Musa Mateja
Mwanamuziki aliyewahi kutikisa kwa miondoko ya TAKEU Afrika Mashariki, Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ (pichani) ameanika wazi kilichomfanya amwage damu hivi karibuni.
Akiongea na gazeti hili ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar, Jumapili iliyopita, Mr Nice alisema kwamba, katika maisha yake hakutegemea kama kuna siku angedai chake na hatimaye kupigwa na kumwaga damu nyingi kiasi kile.
Alisema kuwa, ilikuwa Julai 9, 2010 majira ya saa tano usiku aliondoka nyumbani kwake na kuelekea ndani ya Club ya Masai Kinondoni kwa ajili ya ‘kujirusha’.
Akiwa ndani wa Club hiyo, mara alikutana uso kwa uso na rafiki yake Dj Victor na kuanza kubadilishana mawazo ya hapa na pale na ndani ya maongezi hayo, Nice alijaribu kumtuhumu Dj huyo kuwa, ni mmoja wa jamaa zake wa karibu wanaochangia kuididimiza bendi yake ya Bush.
Akasema hakuishia hapo, aliendelea kumbebesha lawama Dj huyo kwamba, alikwenda kuchukua pesa kwa mama yake ili akamfanyie matangazo mtaani lakini hakufanya hivyo na matokeo yake alikula pesa.
Akizidi kumwaga kweupe chanzo cha timbwili hilo, Mr Nice alisema kuwa, alimpa ukweli jamaa huyo kwamba, hatampa tena kazi
Akasema: “Ndipo jamaa alianza kung’aka kwamba, hapa mjini haishi kwa ajili ya mimi, hivyo nisimtishe kwa lolote, ana uwezo wa kupata kazi pengine na kwamba, kama ni pesa zangu atanirudishia.”
Akiendelea kutoa maneno hayo alisema kuwa, Dj huyo alinyanyuka kwenye kiti na kuanza kulalama huku akielekea nje ya Club hiyo jambo ambalo Nice hakulitilia wasiwasi na kuendelea kugida ‘ulabu’ wake.
Anasema muda ulivyosonga mbele na yeye alitoka nje ambapo alimkuta jamaa akiendelea kupaka na baada ya kumwona Mr Nice alisitisha maongezi na kumfuata, ghafla alimpiga na chupa kwenye paji la uso ambapo alidondoka chini kitendo kilichowafanya watu waliokuwa eneo hilo kusambaa mara moja na kumwacha akiwa amezimia kwa dakika thelathini.
Sakata hilo baada ya kuzua taswira tofauti, baadhi ya wasamaria wema walimnyanyua Mr Nice na kumkimbiza Oysterbay Polisi kwa ajili ya kuripoti na baadaye kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambapo alishonwa nyuzi sita kabla ya kulazwa.
Akiwa Oysterbay, Mr Nice ambaye kwa sasa anatamba na bendi yake ya Bush alifungua jalada la kesi OB/12487/010 kosa likiwa kujeruhiwa na Dj Victor ambaye ametoweka.
BONYEZA HAPA KUPATA HABARI NA BAADHI YA PICHA ZA TUKIO HILO:
CHANZO GLOBAL PUBLISHERS


No comments:
Post a Comment