ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 28, 2010

Mwinyi: Dawa ya Ukimwi isiwapumbaze

Ali Hassan Mwinyi
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, amewataka watanzania wasipumbazwe na taarifa kwamba dawa ya kutibu Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi)imepatikana, waendeleze mapambano dhidi ya ugonjwa huo. 

Mwinyi ameyasema hayo Mweka mkoani Kilimanjaro wakati anazungumza na waandishi wa habari baada ya kuwapokea watu 53 wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Geita (GGM) waliokuwa wamepanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kukusanya fedha za kuwasaidia walioathirika na ugonjwa wa Ukimwi. 

“Tunawahadharisha kwamba kama kweli dawa imepatikana na kuvumbuliwa ni lazima itachukua muda mrefu kuanza kutumika… sasa hapa katikati itakuwaje na je, hapa kwetu itafika lini na ikifika hapo uhai utakuwa unakungojea? Basi tusipumbazike kwa habari hizo,” amesema Alhaj Mwinyi leo.


CHANZO:HABARI LEO

No comments: