ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 29, 2010

Timu ya Houston kupimana nguvu na Wichita,Jumamosi,Aug 7


                Timu ya Houston(Serengeti BoyzClick to view full size image
            Timu ya Wichita(Ngorongoro Heroes)

Timu kabambe ya Houston(Serengeti Boyz) Aug 7 itaelekea Wichita kwa mpambano wa kukata na shoka unaosubiliwa kwa hamu na Wabongo wa huko na vitongoji vyake.

Mara ya mwisho timu hizi kupambana ilikua 2008 huko huko Wichita ambako wenyeji waliibuka na kalamu ya magoli 5-2 zidi ya Houston.

Akiongea na VIJIMAMBO Serengeti Boyz Timu kepteni Alune Mwasabwite,amesema sasa hizi tupo kwenye mazoezi makali na kama unavyojua huu ni wakati wa dozi na kutoa onyo,kama tulivyowafundisha mpira Minnesota(Kili Stars) kwa kipigo cha 6-2 July 4 huko huko kwao ndivyo tutakavyofanya huko huko Wichita.

Wichita timu Kepteni John Cheche akizungumuza na VIJIMAMBO amesema Houston ni wanyela tu kwao na huyo Alune anajua kwamba timu yao kwetu sisi ni sawa na kumsukuma mlevi,wasibweteke na ushindi wa kuwafunga vilema hao wa Minnesota hapa wao wakitia jiwe sisi tunatia chuma tutarudia kipigo kile kile cha umbwa mwizi mpira sio maneno.

Timu za wa West zenyewe zinashindwa kutia mguu,sembuse Houston,tunawasubili mje mchukue vidonge vyenu.
.Mtanange huu unatarajiwa kuanza saa 11 jioni kwenye park ya Redbud mitaa ya 21st na Edgemoor ( 2000 N Edgemoor Wichita,Ks,67202).

No comments: