ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 26, 2010

Chadema wamwekea pingamizi Kikwete

Mgombea urais wa Chadema Dk Slaa
Geofrey Nyang'oro na Lilian Mazula
SHERIA ni msumeno na sasa imgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete atalazimika kufanya kazi ya ziada isimdhuru baada ya Chadema kumwekea pingamizi rais huyo wa serikali ya awamu ya nne.Kikwete alisaini Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa mbwembwe mapema mwaka huu akitaka itumike mwaka huu, lakini Chadema imeitumia sheria hiyo kumwekea pingamizi, ikidai kuwa mgombea huyo wa CCM ameikiuka.
Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Kikwete amekiuka sheria hiyo kwa kwa kutangaza ongezeko la mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma akiwa kwenye mikutano ya kampeni.

"Wanasheria wetu wanashughulikia suala hilo kwa kusaidiana na naibu katibu mkuu, John Mnyika kukamilisha pingamizi hilo na kesho (leo) asubuhi tutawasilisha pingamizi letu kwa msajili wa vyama vya siasa,"KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

No comments: