ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 28, 2010

Jokate, Hasheem

Jelard Lucas na Hemed Kisanda
Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo ameamua kuweka hadharani uhusiano uliopo kati yake na Nyota wa Mpira wa Kikapu anayechezea timu ya Memphis Grizzlier nchini Marekani, Hasheem Thabeeth Manka, Risasi Jumamosi linashuka na ‘makabrasha’ iliyosheheni.

Mlimbwende huyo aliamua kumwaga ‘mchuzi’ baada ya kuwekwa ‘mtu kati’ na waandishi wetu waliomtaka atangaze wazi Hasheem ni nani kwake kufuatia kuwepo kwa uvumi kuwa, wawili hao ni ‘ile mbaya’.

Aidha, minong’ono hiyo ilikuwa ikidai kuwa, Jokate na Hasheem wamekuwa wakikutana kwenye maduka makubwa ya Mlimani City kila mwanamichezo huyo mrefu sana anaporejea nchini Tanzania kwa sababu mbalimbali. 

Kwa mujibu wa watu waliowahi kuwaingiza kwenye macho yao wamesema wawili hao wamekuwa wakionekana sehemu hiyo wakifanya ‘shoping’ mbalimbali kama vile wanatokea nyumba moja.
Akiongea huku wakati mwingine akitoa mifano kwa kutumia mikono na vidole vyake, Jokate alisema kuwa, anamfahamu mcheza mpira huyo kama watu wengine wanavyomfahamu Bongo na si kama ambavyo imekuwa ikivumishwa wao ni wapenzi.

Lakini akatoboa: “Nimekua nikikutana na Hasheem mara kadhaa kila anapokuja Tanzania, wakati mwingine kwa kazi za jamii kwani sisi sote ni watu wa hadhi fulani hapa nchini.”
Akaongeza: “Inashangaza kuona watu wameweza kusema hivyo, lakini mimi kama binadamu ninao uhuru wa kukutana au kuzungumza na mtu yeyote katika nchi hii bila kujali rika lake.” 
Hata hivyo, mnyange huyo alipoteza hali ya kujiamini baada ya kukumbushwa tukio la siku chache zilizopita kuwa, alikuwa na Hasheem kwenye maduka makubwa ya Mlimani City upande wa Samaki ambapo baada ya mazungumzo yao mafupi mlimbwende huyo alisimama kwa dalili za kuondoka.

Aidha, akakumbushwa kuwa, wakati akitaka kuondoka alionekana akibishana jambo na Hasheem huku akimvuta, aliposhindwa kumwinua kitini, yeye alikwenda kuingia ndani ya gari na kuondoka akimwacha Hasheem peke yake.
Jokate alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuweka kweupe kwamba, siku hiyo yeye alikuwa akienda Chuo Kikuu na Hasheem alikuwa akienda mazoezini (hakusema ni wapi).
Akaongeza: “Niliamua kusimamisha gari kwa lengo la kumsalimia kama watu tunaofahamiana tu,” alisema. 

Alipoulizwa kuhusu kutokea kwa mvutano wao wa maneno, Joketi alikataa kutaja sababu ya kuwepo kwa hali hiyo na kusisitiza kuwa, ana mtazamo chanya katika akili yake kuhusu mwanaume hivyo hawezi kuzungumza chochote juu ya jambo hilo kwa siku hiyo ya majadiliano hayo (Alhamisi) mpaka atakapokaa na kushauriana na familia yake. 
“Jamani nashukuru sana, tumezungumza sana lakini kwa sasa siwezi tena kuzungumzia chochote kuhusu Hasheem kwani ni mtu wa kawaida kwangu kama walivyo watu wengine,” alisema.

Akaongeza: “Wakati ukifika na akapatikana mwanaume basi nikimpeleka kwa wazazi huyo ndiyo naweza kumzungumzia, sipendi kwenda kinyume na familia yangu, naomba ‘msinikoti’ kwani wazazi wangu hawapendi kusikia mambo mabaya juu yangu.” 
Chanzo:Global Publishers

No comments: