
Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kuibuka washindi.
WATANI wa jadi katika soka, timu za Simba na Yanga jana walichuana vikali katika mpambano wa Ngao ya Hisani uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mpaka mwisho wa mchezo timu hizo zilitoka sare na kusababisha ipigwe mikwaju ya penati ambapo Simba ‘Wekundu wa Msimbazi’ walifungwa kwa mabao 3-1. Rais wa shirikisho la soka nchini (TFF) Leodgar Tenga (kulia) akimkabidhi Ngao ya Hisani nahodha wa Yanga, Fred Mbuna, baada ya kutwaa ushindi.
Kikosi cha Yanga kilichoanza.
Kikosi cha Simba kilichoanza kuivaa Yanga.
Golikipa wa Simba, Ally Mustapha ‘Bartez’ akidaka moja ya michomo iliyoelekezwa golini kwake.
Sekeseke likiendelea uwanjani na kumkuta beki wa Yanga, Isaac Boakye (kulia), akiwa kama anaswali.
Wakati wa mapumziko na kabla ya mpambano kuanza, wasanii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom walitumia nafasi hiyo kutangaza miaka kumi ya mafanikio tangu kuanza kwa huduma zao hapa nchini.
Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, akipambana na mshambuliaji wa Simba, Shija Mkina.
Golikipa wa Yanga, Yaw Berko akimtoa golini mchezaji wa Simba, Uhuru Selemani, aliyekuwa akilia baada ya kukosa penalti.
Golikipa wa Simba, Ally Mustapha, ilibidi naye aende kuongeza nguvu ya kumbembeleza Uhuru.
Mcheza sinema, Jacqueline Wolper (kushoto) na “shosti” wake ambaye hakufahamika jina mara moja, wakiwa na nyuso za tabasamu baada ya timu yao kushinda.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL










No comments:
Post a Comment