ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 11, 2010

MTOTO WA JOHN RUPIA APIGWA MVUA TATU, ALIPANDA KARANDINGA!

Peter Rupia, akiingia ndani ya Karandika tayari kwenda kuanza maisha mapya gerezani kama alivyonaswa na mpiga picha wetu jana. Askari na jamaa wa mtuhumiwa walikataza kapisa ndugu yao kupigwa picha na wanahabari.
Rupia, akiwa nje ya Mahakama na mawazo tele muda mfupi kabla ya hukumu

MTOTO WA JOHN RUPIA APIGWA MVUA TATU, ALIPANDA KARANDINGA!

Na Joseph Ngilisho,Arusha
MAHAKAMA ya hakimu mkazi mkoani Arusha imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu na miezi mitatu jela Peter Rupia (40) ambaye ni mtoto wa aliye kuwa Katibu mkuu wa kwanza enzi za utawala wa baba wa Taifa ,Mwalimu JK Nyerere, Poul Rupia baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hati ya mashitaka jana mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo,Charles Magesa,mwendesha mashtaka wa serikali, Agustino Kombe, aliieleza mahakama kuwa,mnano tarehe 10 juni mwaka 2008 Peter Rupia akiwa na akili timamu,alijipatia mali kwa njia ya udanganyifu yenye thamani ya shilingi 3,080,000 kutoka kwa mfanyabiashara Rose Mnzava mkazi wa mjini Arusha.

Alisema alichukua vitu mbalimbali vya dukani vyenye thamani hiyo na baadae kukana kutochukua vitu hivyo,kisha kukimbilia jijini Dar ,ndipo mlalamikaji alipoamua kufungua kesi mahakamani baada ya kuona Rupia analengo la kumtapeli.

Vitu vinavyodaiwa kuchukuliwa na mtuhumiwa huyo ni pamoja na Suruali 3,mashati 7,heleni 15,blauzi 3 ,viatu jozi moja na simu tano aina ya Nokia,sonny Erickson, Motorolla,simu aina ya LG na Basicom, vitu hivyo vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 3,080,000.

Akisoma hukumu hiyo,hakimu Magesa alisema kuwa mahakama imemtia hatiani mshitakiwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili

Hakimu Magesa alimhukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitatu na miezi mitatu sanjari na kulipa deni hilo pindi atakapomaliza kutumikia kifungo chake.

Hata hivyo hakimu magesa alimwamuru kukata rufaa iwapo hakuridhika na hukumu hiyo.

Chanzo:Global Publishers

No comments: