ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 17, 2010

MWANAMUZIKI UJERUMANI ASHITAKIWA KWA KUAMBUKIZA UKIMWI MAKUSUDI

Nadja Benaissa
MWIMBAJI wa kike, Nadja Benaissa wa Ujerumani kutoka kundi la No Angels anashitakiwa kwa kufanya ngono zembe wakati kaathirika na virusi vya ukimwi.

Mrembo huyo ambaye ameomba msamaha kupitia kwa mwanasheria wake, anakabiliwa na shutuma za kumwambukiza mwanaume mmoja virusi vinavyosababisha ukimwi mwaka 2004. 

Vilevile anakabiliwa na kosa la kufanya ngono zembe na wanaume wengime wawili zaidi.

Nadja atakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela endapo itadhibitika kwamba alifanya hivyo kwa 
kukusudia.


                    HABARI KWA HISANI YA GLOBAL PAUBLISHERS

No comments: