Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
Na Khadija MngwaiRAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewataka wachezaji waliochaguliwa katika kikosi cha Taifa Stars kufuata kile watakachofundishwa na Kocha mpya Jan Poulsen ili kujenga timu imara.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tenga alisema wachezaji wanatakiwa kuwa na nguvu ya ziada katika kuimarisha nidhamu kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo ya soka kote duniani.
“Wanatakiwa watambue maendeleo ya mpira yanatokana na nidhamu, bidii pamoja na kusikiliza yale mwalimu atakayoyaelekeza. Pia Watanzania wasitarajie mafanikio kuja kama mvua, bali taratibu.
“Ili timu iwe nzuri ni vyema kwa makocha wa klabu zinazoshiriki ligi kuu nchini wakajipanga vema kuwaboresha wachezaji ili iwe rahisi kwa kocha katika kuchagua wachezaji watakaounda kikosi cha taifa,” alisema Tenga.
Aidha Tenga amewataka makocha wazawa kumpa ushirikiano Poulsen ili kuweza kufungua ukurasa mpya wa soka na kuwa na timu bora ya taifa.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment