ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 2, 2010

VURUGU TANGA ZASABABISHA UPIGAJI KURA KUANZA SAA7 MCHANA


Na Dege Masoli, Tanga
MOTO umewaka katika zoezi la upigaji kura za maoni za CCM baada ya kuzuka vurugu kwenye vituo vya kupigiakura na kusababisha zoezi hilo kuanza saa 7 mchana badala ya saa 2 asubuhi.

Aidha katika vurugu hizo ambazo Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Gustav Muba alilazimika kuminyana na wanachama akiamua vurugu hizo zisilete madhara zaidi.

Baadhi ya sababu zilizojiri katika vituo vingi na kusababisha vurugu ni kukosekana kwa majina ya baadhi ya wanachama katika daftari la orodha la kata na lile la wilaya, pamoja na baadhi yao kuzuiwa kupiga kura kutokana na kadi zao kuonesha kuwa sio wananchama hai.

Katika kituo cha mji mwema kata ya Duga upigaji kura ulianza saa7:00 mchana badala ya sa 2:00 asubuhi kama ilivyopangwa baada ya wapiga kura kugoma kuanza kupiga kura kwa madai ya kumtaka mwenyekiti wao wa tawi la mji mwema Mwitike Ramadhani asiwepo katika eneo la kupiga kura madai kuwa huenda akahujumu zoezi hilo.

Hali hiyo ilimlazimu mwenekiti wa Mkoa wa chama hicho Gustav Muba kuzunguka katika vituo mbalimbali ambapo alifika katika kituo hicho majira ya saa 6:00 mchana na kuamuru mwenyekiti huyo aondoke ndipo upigaji ukaanza majira ya saa 7:00 mchana.



Aidha taarifa zilizopatikana kituoni hapo zilidai kuwa, makatibu watatu wa matawi wa chama hicho katika hiyo walifukuzwa kazi kwa tuhuma za kufanya mchezo mchafu wa kutoa kadi kwa wanachama wapya ambao hawajajadiliwa na kamati ya siasa.



Makatibu waliofukuzwa kazi na uongozi wa Mkoa wa chama hicho ni Jackson Mbai wa tawi la mji mwema, Mohamed Lukindo Duga kaskazini B na Erena Barua wa tawi la Duga kaskazini A

Katika kituo cha Msambweni B, hali ilikuwa hiyohiyo, ambapo zoezi la uchaguzi lilisimama kwa saa kadhaa kabla ya Katibu wa mkoa kufika ambapo alituliza vurugu hizo huku mmoja ya wagombea nane wa nafasi ya udiwani kata ya msambweni Godfrey Robert akipandwa na jazba kwa kitendo cha katibu huyo kutengua baadhi taratibu ili uchaguzi huo uendelee


                                              PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS

No comments: