Advertisements

Thursday, September 9, 2010

Bomu latikisa uwanja wa ndege Mogadishu

Takriban watu wanane wamefariki dunia katika shambulio la bomu na tukio la kufyatuliana risasi katika uwanja mkuu wa ndege mjini Mogadishu.
Maafisa wa uwanja wa ndege walisema, wapiganaji walianza kufyatua risasi kwa majeshi ya kutunuza amani ya Umoja wa Afrika AU baada ya mlipuko wa mwanzo.
Taarifa zisizothibitishwa zimeeleza kuwa majeshi ya AU na wapiganaji waliuawa katika shambulio hilo.
Kundi la al-Shabab , linalopambana na serikali kwa nia ya kutaka kudhibiti nchi hiyo, imeripotiwa kuwa limejitangaza kuhusika na shambulio hilo.
Maafisa wa uwanja wa ndege wameiambia BBC kwamba majeshi ya AU yalisimamisha gari la kwanza lililokuwa likielekea kwenye lango kuu la uwanja huo.
Gari hilo lililipuka, na muda mfupi baadae wapiganaji waliwasili katika gari jingine na kuanza kufyatua risasi.
Maafisa walisema wapiganaji kadhaa wameuawa, pamoja na Msomali mmoja aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la ndege la kibinafsi.
Uwanja wa ndege wa Mogadishu, ambao ni muhimu sana, ni moja ya maeneo machache katika mji mkuu huo yanayodhibitiwa na jeshi la AU na serikali.

No comments: