ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 8, 2010

KIFO CHA P DIDDY: MAIMATHA APATA PIGO!

Kifo cha Perfect Kasiga, maarufu kwa jina la P. Diddy, kimeacha pigo kubwa kwa mchumba wake, Maimatha Jesse ambaye tangu kupewa taarifa za kifo chake, amekuwa akilia kwa uchungu na kukumbuka walikotoka kwa kusema kuwa alimpenda sana P. diddy na alibadili dini kwa ajili yake. Pichani ni Maimamatha kama alivyokutwa na mtandao huu msibani Kinondoni jijini Dar es salaam akilia kwa uchungu na kufanya marafiki na ndugu nao kuangua kilio kila wakati. 
...rafiki wa karibu wa Mai akilia kwa uchungu
...mama wa marehemu (aliyekumbatiwa) akilia kwa uchungu
...huzuni yatawala nyumbani kwa marehemu
Pichani (kushoto) ni marehemu P. Didy enzi za uhai wake. Picha hii alipiga mwaka huu katika Hoteli ya The Atriums, iliyopo Sinza jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Bendi ya Diamond Musica, Judith Mosha, ambaye walikuwa wakiendesha naye bendi hiyo iliyoanza kujipatia umaarufu nchini.

BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE-AMEEN!

PICHA: ISSA MNALLY/MAKTABA/GPL


FLASH BACK........................................

BAADA YA HIVI KARIBUNI 'KUKWARUZANA' NI JUZI TU WALISAMEEANA.


Lile sakata ambalo hivi karibuni lilichukua nafasi katika ‘midia’ nyingi la Mtangazaji wa Televisheni ya Taifa, TBC1, Maimartha Jesse na mpenzi wake Perfect Kasiga ‘P.Didy’ kufikishana polisi, hatimaye limefikia tamati kwa wawili hao kuamua kusameheana.

Wakiongea na Ijumaa Wikienda kwa nyakati tofauti juzi, mastaa hao wasioisha kutifuana wamesema kuwa, yaliyotokea yametokea na kwamba, wameamua kumwachia Mungu ili kila mmoja aweze kuendelea na maisha yake.

Wa kwanza kuongea na Mwandishi Wetu alikuwa ni Maimartha ambaye alisema kuwa, licha ya mpenzi wake huyo kumuadhiri kwa kumpiga kisha kumuweka ndani, ameona bora wayamalize ili kujiweka safi mbele ya jamii.

Alisema kuwa, kwa kila alilofanyiwa na P.Didy anamuachia Mungu lakini kwa upande wa uhusiano wa kimapenzi, inabidi waende likizo kwanza.

“Tumesameheana, mimi nimefuta kesi niliyomfungulia na yeye pia ameifuta aliyonifungulia, tumeamua kumuachia Mungu lakini kwa upande wa uhusiano wetu, hatujarudiana,”alisema Mai.

Naye P. Didy ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Bendi ya Diamond Musica ‘Vijana Classic’ alipotafutwa na kuulizwa juu ya ishu hiyo ya kusameheana alisema; “Mimi naogopa kuweka mambo binafsi hadharani ila ni kweli tumesameheana, kesi nimeifuta na kila mtu anaendelea na mambo yake. Kama alivyosema yeye anamuachia Mungu na mimi pia namuachia Mungu”.

Awali, Maimartha alimfungulia P.Didy kesi katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa kumshushia kipigo kabla ya P.Didy naye kumfungulia Maimartha kesi akimtumtuhumu kumvunjia duka lake kisha kuiba. 

No comments: