Kiwanja cha kufurahisha watoto cha kibirizi wilaya ya Chake Chake,Mkoa wa Kusini,Pemba,Zanzibar
Na Saleh Mohammed Washington DC,Sept 7,2010
Kama sehemu inayooneka katika picha, kiwanja cha kufurahisha watoto leo vimekuwa vya kutisha watoto
Katika picha ni kiwanja cha kufurahishaia watoto ambacho kipo kibirizi wilaya ya chake chake, mkoa wa kusini Pemba, Zanzibar,Tanzania, viwanja hivi vipo viwili tu zanzibar, kimoja kipo pemba na chengine kipo unguja, ni viwanja vilivyojengwa katika mwanzoni mwa miaka ya sabini, vilikuwa viwanja pekee vilivyokuwa na mvuto na vyenye kufurahisha watoto kwa Afrika mashariki na kati, kwa wakati huo vilikuwa na hadhi sawa na baadhi ya nchi za ulaya.
vifurahisho kama vile merry go round, train iliyokuwa na mzunguko ambao uliwafanya watoto kufurahia trip zao, wounder wheel hili ni jipembea moja kubwa lililo naumbile la duara kama gurugumu ambalo kama utaa eneo lililotambarare uawezakuliona hata maili kwa tano.
Gari ilikuwa kifurahisho cha kwanza kinacho tembelewa na watoto, barabara yake imejengwa juu kwa juu ili uweze kupanda gari unaweza kutumia siku yako yote kuwa katika mstari wa kufika kupanda hizo gari, sio hiyo inayoonekana hapo pichani, hizo zinatembea juu kwa juu.
Zanzibar ni moja ya nchi zilizokuwa na mvuto mkubwa kuanzania jina lake, kiuchumi, hulka na hata kiutamaduni na watu wake, katika miaka ya sabini serikali ya Zanzibar chini ya rais wa Zanzibar Abeid Aman karume aliweza kuijenga na kuiweka katika viwango vya kimataifa na kiweka katika rekodi katika Afrika, leo kila kitu kimetoweka, kunani Zanzibar?
No comments:
Post a Comment